13.9 C
New York

Mkutano wa siasa wasababisha vifo 39

Published:

MUMBAI, India
WATU 39 wamepoteza maisha na wengine 51 kujeruhiwa katika tukio la kukanyagana lililotokea wakati wa mkutano wa siasa Kusini mwa India.
Kwa mujibu wa taarifa, miongoni mwa waliofariki ni watoto na ni tukio lililotokea katika Jimbo la Tamil Nadu.
Chanzo cha mkanyagano huo ni idadi kubwa ya wananchi waliofurika katika mkutano wa mwanasiasa mpya aliyetokea katika tasnia ya filamu Vijay.
Katika video za mkutano huo, mamia ya wananchi walionekana wakiwa wamepoteza fahamu kutokana na kukosa hewa ya kutosha.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa kati ya waliofariki, 17 ni wanawake, 13 ni wanaume, huku tisa wakiwa ni Watoto.
Mmoja ya mashuhuda wa tukio hilo, anasema: “Watoto wawili wa kaka yangu walikuwa pale. Vijana wa kiume. Mkubwa amefariki na mdogo hajulikani alipo. Ndugu zangu, shimeji yangu nao wako kwenye chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). Nifanyeje?”
Kupitia mitandao ya kijamii, Vijay ameeleza kusikitishwa na tukio hilo akisema ni taarifa za kuumiza na kuhuzunisha.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img