13.4 C
New York

Man United yavunja rekodi mapato ya mwaka

Published:

MANCHESTER, Uingereza
LICHA ya kutokufanya vizuri uwanjani, klabu ya Manchester United imevunja rekodi ya mapato yake baada ya kukusanya Pauni milioni 666.5 kwa mwaka jana.
Ndani ya uwanja, Man United ilimaliza msimu uliopita ikiwa nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi Kuu ya England (EPL).
Hata hivyo, licha ya majanga hayo, bado ilikusanya Pauni miloni 333.3 kutokana na mkataba wake na kampuni Snapdragon.
Kama hiyo haitoshi, mapato ya viingilio vya mechi yalifikia Pauni milioni 160.3, kiasi ambacho hakijawahi kupatikana klabuni hapo.
Akizungumzia mafanikio hayo ya kiuchumi, Mtendaji Mkuu, Omar Berrada, alisema: “Kuvunja rekodi ya mapato ndani ya kipindi kigumu ndani ya uwanja ni kielelezo cha ubora wa Manchester United. Kwa msimu huu wa 2025-26, tutaangalia namna ya kuboresha maeneo mbalimbali.”
Kwa upande mwingine, hatua ya kupunguza wafanyakazi kutoka 1,100 hadi 700 kwa miaka miwili ya hivi karibuni imetajwa kuchangia mafanikio hayo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img