13.4 C
New York

Mechi tatu kuamua hatima ya Ruben Amorim?

Published:

MANCHESTER, Uingereza
IMERIPOTIWA kuwa matokeo ya mechi tatu zijazo ndiyo yatakayoamua hatima ya kibarua cha kocha wa Manchester United, Ruben Amorim.
Man United inasota msimu huu ikiwa nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi Kuu baada ya kukusanya pointi nne pekee katika mechi nne.
Tangu alipokabidhiwa mikoba, kocha huyo raia wa Ureno ameshinda mechi nane pekee kati ya 31 za Ligi Kuu alizokaa kwenye benchi.
Licha ya mabosi kusema wanamuunga mkono, taarifa zinaeleza kuwa huenda wakamgeuka endapo Man United haitafanya vizuri katika mechi tatu zijazo.
Man United watakuwa nyumbani Jumamosi ya wiki hii kuwakaribisha mabingwa wa Kombe la Dunia kwa ngazi ya Klabu, Chelsea.
Baada ya mchezo huo, itasafiri kwenda ugenini kwa mchezo dhidi ya Brentford, kabla ya kurejea Old Trafford kumenyana na Sunderland.
Makocha wanaohusishwa na kibarua chake kwa sasa ni Oliver Glasner, Gareth Southgate, Marco Silva, Andoni Iraola na Mauricio Pochettino.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img