BENFICA, Ureno
HAITASHANGAZA kuona kocha wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp, akiajiriwa kuliongoza benchi la ufundi la Benfica.
Ndiyo, mmoja ya wagombea wa nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi ujao klabuni hapo ameahidi kumuajiri Mjerumani huyo.
Klopp mwenye umri wa miaka 58, amekuwa nje ya kazi tangu alipoondoka Anfield mwishoni mwa msimu wa 2023-24.
Kwa sasa, amekuwa akifanya kazi kama mshauri wa masuala ya soka katika kampuni ya Red Bull inayomiliki klabu za RB Leipzig na RB Salzburg.
Aidha, Cristovao Carvalho ambaye ni mgombea wa kiti cha urais pale Benfica, amesema Klopp atatua klabuni hapo endapo atachaguliwa.
Mbali ya hilo, pia Carvalho amedai kuwa klabu hiyo itafika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ndani ya miaka mitatu tu ya uongozi wake.
Published:


