15.8 C
New York

Yamal, De Jong kuikosa Newcastle

Published:

CATALUNYA, Hispania
KOCH wa Barcelona, Hansi Flick, amefichua kuwa atamkosa mshambuliaji wake, Lamine Yamal, katika mchezo wa Alhamisi ya wiki hii dhidi ya Newcastle United.
Wakati huo huo, Barcelona itaikabili Newcastle katika mchezo huo wa hatua ya makundi ikiwa haina kiungo wake, Frenkie de Jong, ambaye pia aliumia akiwa na Uhonalzi.
Yamal mwenye umri wa miaka 18, amekosekana katika mchezo wa leo wa La Liga dhidi ya Valencia baada ya majeraha aliyopata akiwa na timu ya taifa ya Hispania.
Nyota huyo alicheza mechi zote mbili za Hispania za kufuzu Kombe la Dunia, akizikabili Bulgaria na Uturuki.
Msimu huu umeanza vizuri kwake kwani amefunga mabao mawili na kutoa ‘asisti’ tatu katika mechi za Barca, pia akiingia kambani mara tatu akiwa na Hispania.
“Atakosekana (dhidi ya Newcastle). Aliitumikia Hispania akiwa na maumivu na hakufanya mazoezi,” alisema Flick.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img