LONDON, Uingereza
WAKATI Chelsea ikilazimishwa sare ya mabao 2-2 na Brentford jana, hali ilikuwa mbaya kwa Waziri Mkuu wa Uingereza aliyekuwa uwanjani akifuatilia mchezo huo wa Ligi Kuu.
Baadhi ya mashabiki wa Blues walionekana wakiimba kwa kulikashifu jina la kiongozi huyo.
Tukio hilo linatokea wakati huu Serikali ya Uingereza ikiwa kwenye shinikio la maandamano makubwa ya wananchi wanaopinga wahamiaji haramu.
Waziri huyo, Keir Starmer, amekuwa na wiki mbaya kwani siku chache zilizopita alizomewa na mashabiki wa timu ya taifa ya England ‘Three Lions’ katika mchezo wao dhidi ya Andorra.
Hata kabla ya mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Aston Villa mjini Birnigham, mashabiki walionekana wakiwa na mabango yenye jumbe za kupinga wahamiaji haramu.
Baada ya mchezo huo, kocha wa England, Thomas Tuchel, alisema hakusikia sauti hizo lakini hakubaliani nazo.
Keir anafahamika kuwa ni shabiki mkubwa wa Washika Bunduki wa Kaskazini mwa Jiji la London, Arsenal, na alikuwa uwanjani wakati timu hiyo ikimenyana na Nottingham Forest wikiendi hii.
Published:


