9.8 C
New York

City wamalizana na Donnarumma, kumng’oa Ederson

Published:

PARIS, Ufaransa
MLINDA mlango wa PSG na timu ya taifa ya Italia, Gianluigi Donnarumma, amekubaliana masilahi binafsi na klabu ya Manchester City.
Donnarumma mwenye umri wa miaka 26, amefikia hatua hiyo akiwa amezuiwa kujumuhika na wenzake katika kikosi cha PSG.
Kwa mujibu wa taarifa, aliamua kujiweka kando baada ya mabosi wa klabu hiyo kumwambia kuwa kipa mpya, Lucas Chevalier, ndiye atakayekuwa chaguo la kwanza kikosini.
Kile kilichoelezwa na mwandishi wa habari wa Italia, Fabrizio Romano, ni kwamba kuna mazungumzo yanayoendelea kati ya PSG na Man City.
Aidha, ripoti za vyombo vya habari vya Ufaransa zinaeleza kuwa dili hilo linaweza kuwagharimu mabosi wa Etihad kiasi cha Pauni milioni 43.
Kuingia kwa Donnarumma kunafungua milango kwa kipa chaguo la kwanza wa Man City, Ederson, ambaye huenda akatimkia Galatasaray.
Ederson aliishia benchi na kumtazama kipa mpya, James Trafford, akicheza dakika zote 90 za mchezo uliopita dhidi ya Tottenham, ambao hata hivyo ulimalizika kwa Man City kufungwa mabao 2-0.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img