14.7 C
New York

Nini kujadiliwa Mkutano wa Trump, Putin?

Published:

LOS ANGELES, Marekani
RAIS wa Marekani, Donald Trump, atakutana na mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin, mwishoni mwa wiki hii. Mkutano huo utafanyika Ijumaa ya Agosti 15 mjini Alaska, Marekani.
Huu ni mwendelezo wa viongozi hao kukutana, kama walivyofanya mara kadhaa wakati wa awamu ya kwanza ya Rais Trump madarakani.
Safari hii, kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, ajenda kuu ni namna ya kumaliza vita inayoendelea kati ya Urusi na majirani zao, Ukraine.
Kabla ya Uchaguzi uliomrejesha madarakani, Rais Trump alisema angeimaliza vita hiyo ndani ya saa 24 tu baada ya kuchaguliwa, lakini zimeshapita siku takribani 200 tangu alipoingia Ikulu.
Kwa mujibu wake, kukutana na Rais Putin kutaongeza kwa kiasi kikubwa kasi ya kumaliza vita hiyo.
Je, Rais Trump anahitaji nini kupitia Mkutano huo utakaofanyika Alaska, Mji uliopo Kaskazini-Magharibi mwa Marekani?
Ndoto kubwa aliyonayo ni kuona akiandika historia ya kuwa mtu pekee aliyefanikiwa kuzima vita ya majirani hao. Rais Trump anataka kuthibitisha kuwa anastahili tuzo ya Amani ya Nobel, kama alivyopendekeza mshirika wake mkubwa na Rais wa Israel, Benjamin Netanyahu.
Katika jitihada zake hizo, Rais Trump amesema anaangalia uwezekano wa kuwakutanisha kwenye meza ya mazungumzo ‘mahasimu’ wawili, Rais Putin na mwenzake wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy.
Je, Rais Putin anahitaji nini katika Mkutano wake na Trump wiki hii? Makala haya yanaendelea kuchambua.
Rais Putin, kama ambavyo amekuwa akisisitiza, atataka (Rais Trump) kumhakikishia kuwa maeneo yote waliyoteka Urusi wakati wa vita dhidi ya Ukraine yanabaki kuwa mali yao.
Ifahamike kuwa jeshi la Urusi linashikilia miji mikubwa minne ya Mashariki mwa Ukraine; Donetsk, Luhansk, Kherson na Zaporizhzhia.
Kwa upande mwingine, Rais Putin atamtaka Rais Trump kumhakikishia kuwa Marekani itapiga kura ya kutokuunga mkono uanachama wa Ukraine ndani ya NATO.
Ikumbukwe kuwa uanachama wa NATO unaifanya Ukraine isaidiwe na washirika wake ndani ya Umoja huo, zikiwamo Marekani, Ufaransa na Uingereza.
Hivyo, ni rahisi kusema Rais Putin atatumia Mkutano wake na Rais Trump kumuomba uwezekano wa wanajeshi wa NATO kuondoka katika ardhi ya Ukraine.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img