8 C
New York

Polisi Babati yawafikia vijana  wakaa vijiweni, wacheza pool table

Published:

Na Mwandishi Wetu

Jeshi la Polisi Wilaya ya Babati mkoani  Manyara limewataka vijana kuacha tabia ya kukaa vijiweni na kucheza pool table asubuhi badala yake wajishughulishe na kazi halali za kujipatia kipato ili kuepuka kujiingiza katika matukio ya uhalifu

Wito huo umetolewa na Polisi Kata ya Duru Wilaya ya Babati,  Mkaguzi wa Polisi Fadhil Mgeta , Julai 21, 2025 wakati akitoa elimu ya madhara ya kukaa kijiweni bila kufanya kazi kwa vijana  katika Kijiji cha Qatadium Kata ya Duru.

Pia ametoa onyo kwa vijana hao kuacha kujihusisha na matukio ya uhalifu kwani ni kosa la jinai na Jeshi la Polisi halitavimilia mtu au watu watakaobainika.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img