8 C
New York

Madai ya dada wa Polepole , Polisi yachunguza 

Published:

Na Mwandishi Wetu

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam  limesema limepokea taarifa za kuchukuliwa na watu asiowafahamu na  kurejeshwa  kwa mwanamke aliyejitambulika kwa jina la Christina  Polepole, mwenye umri wa miaka 52, mkazi wa Bahari Beach, mtaa wa Katumba, Kinondoni.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa leo  Julai 18,2025 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro tukio hilo lilianza kuripotiwa kupitia mitandao ya kijamii mnamo Julai 17, 2025, ambapo mtu aliyejitambulisha kwa jina la Humphrey Polepole akijieleza kuwa  dada yake alichukuliwa na watu wasiojulikana waliovamia nyumba yake kwa kuruka ukuta.

“Dada huyo alifika mwenyewe katika kituo cha Polisi Kawe na kutoa taarifa  kuwa jana  alichukuliwa  na watu ambao hakuwafahamu na baadae walimrudisha nyumbani kwake jana hiyohiyo,” ameeleza Muliro.

Jeshi hilo limethibitisha kuwa linaendelea kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo kwa kushirikiana na wananchi pamoja na vyombo vingine vya usalama, huku likitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati taratibu za uchunguzi zikiendelea.

Aidha Kamanda Muliro amesema kwa kushirikiana na wananchi Jeshi la Polisi linaendelea kuimarisha usalama katika jiji la Dar es Salaam.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img