25.2 C
New York

Twiga Stars yaanza vibaya WAFCON

Published:

BERKANE, Morocco
TIMU ya soka ya Wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) imepoteza kwa kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Mali katika mchezo wa fainali za Mataifa Afrika (WAFCON).
Mchezo huo wa kwanza kwa kila timu ni wa Kundi C na ulichezwa katika Uwanja wa Berkane.
Mali walipata bao pekee hilo zikiwa zimebaki sekunde chache kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika, mfungaji akiwa ni Saratou Traore.
Kwa ushindi huo, sasa Mali inafikisha pointi tatu, sawa na mabingwa watetezi, Afrika Kusini, ambao waliibamiza Ghana mabao 2-0 katika mchezo wa mapema.
Kwa upande mwingine, Twiga Stars itakuwa na nafasi ya kurudi kivingine itakapoivaa Afrika Kusini katika mchezo wa Ijumaa ya wiki hii.
Mechi hiyo itatanguliwa na ile ya Mali kutoana jasho na Ghana, ambayo nayo itajaribu kupata ushindi wa kwanza kwenye michuano hiyo.

Related articles

Recent articles