9.2 C
New York

Rais Samia azindua Daraja la JP Magufuli

Published:

Na Mwandishi Wetu

Rais Samia Suluhu Hassan leo Juni 19, 2025 amefungua rasmi Daraja la  John Pombe Magufuli (Kigongo – Busisi) lililopo mkoani Mwanza, ili lianze kutumika  bade ya kukamilika  kwa asilimia 100.

Daraja hilo linaunganisha Wilaya ya Misungwi kupitia eneo la Kihongo na Wilaya ya Sengerema kupita eneo la Busisi, likiwa na urefu wa kilomita tatu pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa kilomita 1.66.

Ujenzi wa daraja hilo uliasisiwa na Hayati Magufuli na aliyefariki Machi 17, 2021 likiwa limefikia asilimia 24.6 za utekelezwaji wake na mrithi wake, Rais Samia  aliendeleza na hatimaye kukamilisha.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img