23.1 C
New York

Dar yatajwa kinara watoto wa mtaani

Published:

Na Mwandishi Wetu

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, imeitaja Dar es Salaam kuwa Mkoa unaongoza kwa  kuwa na watoto wengi wanaoishi na kufanya kazi mtaani ni Dar es Salaam,ikifuatiwa na Dodoma.

Kauli hiyo imetolewa  leo Mei 27,2025 bungeni na Waziri wa Wizara hiyo,Dk Dorothy Gwajima wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.

Ameitaja mikoa mingine  kuwaitiani ni Mwanza, Mbeya, Arusha na Iringa huku Mikoa inayoongoza kuchangia maeneo ya miji kuwa na watoto zaidi ni Kagera, Geita, Kigoma, Dodoma, Mwanza na Shinyanga. 

Amesema katika kipindi cha mwezi Julai 2024 na Aprili 2025, watoto 10,782, wakiwemo wakiume 6,108 na kike 4,674 wanaoishi na kufanya kazi mitaani waliokolewa kutoka mazingira ya mtaani.

Vilevile, Wizara imeandaa Kanuni za Utendaji (Standard Operating Procedure – SOP) za namna ya kushughulikia changamoto za Watoto waishio na kufanya kazi mtaani.

Aidha amesema  kufikia mwezi Aprili mwaka huu, migogoro ya ndoa 97,234 ilikuwa imepokelewa kupitia Kitengo cha Ustawi wa Jamii katika ngazi ya halmashauri na Taifa ambapo kati ya hiyo, 81,820 ilipatiwa ufumbuzi na 15,414 ilipelekwa mahakamani kwa hatua zaidi.

Dk.  Gwajima amesema katika mwaka wa fedha 2025/2026 wizara yake itatekeleza vipaumbele vitano ikiwa ni pamoja na kukuza ari ya jamii kushiriki katika kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo iliyoibuliwa.

 Ameongeza kuwa wizara hiyo itaratibu na kutoa huduma za ustawi na maendeleo ya jamii ikiwa ni pamoja na kutokomeza vitendo vya ukatili, na uwezeshaji wanawake kiuchumi.

Waziri huyo ameomba kupitishiwa bajeti ya jumla ya Sh76 bilioni kwa mwaka wa fedha wa 2025-2026.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img