21 C
New York

Dk. Biteko afanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Morocco

Published:

Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko ametembelea Bunge la Morocco ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi nchini humo.

Akiwa Bungeni hapo, Dk Biteko amefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la nchi hiyo, Rachid Talbi El Alami na Naibu Spika, Lahcen Haddad katika ofisi za Bunge hilo zilizoko jijini Rabat nchini Morocco.

Akiwa Bungeni hapo, Dk. Biteko amefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la nchi hiyo, Rachid Talbi El Alami na Naibu Spika, Lahcen Haddad katika ofisi za Bunge hilo zilizoko jijini Rabat nchini Morocco.

Pamoja na mambo mengine, wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizo mbili hususan katika sekta ya nishati, kilimo, viwanda na biashara.

Katika ziara hiyo nchini Morocco, Biteko ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dennis Londo, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Ally Mwadini, wataalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC).

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img