16.6 C
New York

Makamu wa Rais Mstaafu Afrika Kusini afariki

Published:

PRETORIA, Afrika Kusini

ALIYEWAHI kuwa Makamu wa Rais wa Afrika Kusini, Phumzile Mlambo-Ngcuka, amefariki akiwa na umri wa miaka 71. Ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo nchini humo.

Katika taarifa iliyotolewa na familia yake, Phumzile alifariki juzi Ijumaa, Novemba 20, 2026, akiwa anaendelea na matibabu.

Phumzile alikuwa Makamu wa Rais wa Afrika Kusini kuanzia mwaka 2005 hadi 2008, wakati huo pia akiwahi kuwa Waziri wa Madini na Nishati.

Kwa upande mwingine, aliwahi kufanya kazi kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa [UN].

Pia, aliwahi kuwa Mkuu wa Shirika la Wanawake la UN akishughulikia masuala ya usawa wa kijinsia kuanzia mwaka 2013 hadi 2021.

Miongoni mwa walioeleza kusikitishwa na taarifa za kifo chake ni Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres, aliyetumia ukurasa wake wa X kumtaja Phumzile kama bingwa wa harakati za kuwakomboa mabinti na wanawake duniani.

Related articles

Recent articles