16.6 C
New York

Iwobi aweka rekodi akiizima Man City

Published:

LONDON, Uingereza

KIUNGO wa Fulham, Alex Iwobi, amefikisha mechi 100 za Ligi Kuu ya England [EPL] akiwa kikosi cha kwanza wakati timu hiyo ilipopata sare ya bao 1-1 mbele ya Manchester City katika mchezo wa leo Novemba 21, 2026.

Iwobi raia wa Nigeria, alijiunga na Fulham mwaka 2023 akitokea Everton na leo alikuwa sehemu ya kikosi kilichoanza dhidi ya Man City.

Hata hivyo, nyota huyo hakumaliza kwani alitolewa zikiwa zimebaki dakika 20 na kumpisha Antonee Robinson.

Hivyo, Iwobi anakuwa mchezaji wa kwanza wa Afrika kufikisha mechi 100 za Ligi katika historia ya Fulham.

Kwa ujumla, nyota huyo wa zamani wa Arsenal na Everton amecheza jumla ya mechi 122 za Ligi tangu alipojiunga na Fulham. Amefunga mabao 20 na ‘asisti’ 12.

Related articles

Recent articles