11.9 C
New York

Jela inamsubiri kwa kuvunja sanamu la Yesu

Published:

VILNIUS, Lithuania

RAIA wa Uingereza, Aaron Goodfellow, ameingia matatani akiwa nchini Lithuania baada ya video inayomuonesha akiwa amevunja sanamu la Yesu katika kanisa moja mjini Vilnius.

Goodfellow [37], alinaswa na kamera za usalama [CCTV] akiwa amelibeba sanamu hilo lililotengenezwa kwa Mbao na ghafla liling’oka mikono.

Licha ya Mchungaji wa kanisa hilo, Elijas Anatolijus Markauskas, kutangaza kumsamehe, raia huyo wa kigeni hayuko salama linapokuja suala la sheria kwani anaweza kumuhukumu kifungo cha miaka mitatu gerezani.

“Naamini Mungu anampenda [Goodfellow] na atamsamehe. Kwa upande wangu, pia nimemsamehe,” amesema Mchungaji Markauskas.

“Nampa baraka zote Aaron na ni matumaini yangu kwamba ataelewa namna kitendo chake kilivyoumia watu wengi wanaoamini kuwa msalaba ni alama ya uokovu.”

Baada ya video hivyo kusambaa mitandaoni, mamlaka za Lithuania zilisitisha hati ya kusafiria ya Goodfellow, huku polisi wakiendelea na uchunguzi.

Kwa upande mwingine, vyanzo vya habari vimeripoti kuwa Goodfellow ni meneja wa mgahawa mmoja wa Kiitaliano nchini Uingereza, ajira ambayo ana miezi michache tu tangu aianze.

Related articles

Recent articles