12.9 C
New York

Baada ya kutoswa, Conte aichokoza United

Published:

MILAN, Italia

KOCHA wa zamani wa Chelsea, Antonio Conte, amedai kuwa klabu yoyote inayohofia kumpa ajira, basi imechagua kupishana na makombe.

Conte amekuja na kauli hiyo alipoulizwa juu ya Man United kumchukua Mauricio Pochettino wakati yeye ndiye aliyekuwa akihusishwa zaidi na kibarua hicho.

“Mara yao ya mwisho kuwa mabingwa wa Ligi ni mwaka 2013, wakati huo wakiwa chini ya Ferguson. Namuheshimu mno Alex Ferguson,” amesema Conte.

Muitalia huyo alikuwa kwenye rada za Man United kwa muda mrefu lakini mabosi wa klabu hiyo walichagua kwenda na Pochettino aliyekuwa akiinoa timu ya soka ya Taifa ya Marekani.

Kwa sasa, Conte mwenye ‘CV’ kubwa ya kufanya kazi na Juventus, Inter Milan na Tottenham, hana kibarua kwani alishaachana na Napoli.

Related articles

Recent articles