20.2 C
New York

England yapewa Haaland; Yamal na Mbappe vita nzito

Published:

LONDON, Uingereza

DROO ya hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya [Nations League] ilichezeshwa jana Novemba 20, 2026, ambapo Norway ya Erling Haaland imeangukia kwa England.

Mechi nyingine kali ya robo fainali ni ile itakayowakutanisha mabingwa wa Kombe la Dunia, Hispania, dhidi ya Ufaransa ya Kylian Mbappe.

Wakati huo huo, robo fainali nyingine kali itazikutanisha Uholanzi na Ureno, huku Ubelgiji ikiumana na mabingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2014, Ujerumani.

Hivyo, mshindi kati ya Uholanzi na Ureno atakutana na mbabe wa mechi kati ya Hispania na Ufaransa katika hatua inayofuata ya nusu fainali.

Hivyo hivyo, mshindi kati ya Ujerumani na Uholanzi ataingia nusu fainali kucheza na mbabe wa mechi inayozikutanisha Norway na England.

Wakati huo huo, zipo mechi za ‘play-off’ kati ya Bosnia na Denmark, Hungary v Serbia, Ireland v Croatia, Slovenia v Wales, Cyprus v Macedonia, Estonia v Romania, Faroe v Georgia, na Belarus v Israel.

Related articles

Recent articles