LONDON, Uingereza
KAMA mabosi wa Tottenham watakwama kumbakiza winga wao wa Kibrazil, Richarlison, basi hawatomuuza kwa klabu yoyote ya Ligi Kuu ya England [EPL].
Richarlison [29], anatarajiwa kuondoka klabuni hapo baada ya kuona amepoteza nafasi ya kuanza katika kikosi cha kocha Roberto De Zerbi.
Mkataba wake na klabu hiyo ya Kaskazini mwa London umebakiza chini ya mwaka mmoja na tayari Everton na Crystal Palace zinapigana vikumbo kuiwania saini yake.
Wakati huo huo, vigogo wa Kaskazini mwa London, Arsenal, kama ilivyo kwa majirani zao wa Magharibi, Chelsea, nao wanajaribu kumpigia hesabu.
Kuelekea dirisha dogo la usajili wa Januari, 2026, klabu za Italia na Hispania nazo zimeonesha kuitaka huduma yake, ingawa pia anahusishwa na mpango wa kutimkia Saudi Arabia.


