DAKAR, Senegal
CHAMA talawala cha Senegal, Pastef, kimemfuta uanachama Rais wa nchi hiyo, Bassirou Diomaye Faye, sambamba na wanachama wengine 31.
Hatua hiyo inaendeleza mvutano uliodumu kwa muda mrefu kati ya Rais Faye na kiongozi wa Pastef, Ousmane Sonko, ambaye pia ndiye Spika wa Bunge.
Wawili hao waliowahi kuwa marafiki wakubwa, wamekuwa ‘chui na paka’ baada ya Faye kumfuta kazi Sonko aliyekuwa Waziri Mkuu wake.
Ni kutokana na uhasama huo, Rais Faye kwa kushirikiana na baadhi ya vigogo wa Serikali yake, waliunda Chama chao, Kiiray Republican Patriots.
Hata hivyo, bado Sonko ana ushawishi mkubwa kwa kuwa Chama anachokiongoza, Pastef, ndicho chenye nguvu, ambapo kina wawakilishi 130 kati ya 165 walioko bungeni.


