7.3 C
New York

Waasi DR Congo waua raia 44

Published:

KINSHASA, DRC

MASHAMBULIZI yaliyofanywa na waasi wanaohusishwa na Kundi la Islamic State [IS] yamesababisha raia 44 kupoteza maisha Kaskazini-Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo [DRC].

Taarifa zinaeleza kuwa mashambulizi hayo ya wiki hii ni tofauti na yale ya Jimbo la Ituri, ambapo watu wenye silaha waliua raia wasio na hatia wapatao 66.

Jimbo hilo linafahamika kuwa ni kitovu cha mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, ikielezwa kuwa wataalamu wa afya watatu nao waliuawa katika shambulizi hilo.

Hivi karibuni, Shirika la Afya la Kimataifa [WHO] liliweka wazi kuwa mapigano yanayoendelea kati ya waasi na jeshi la Serikali ni kikwazo katika makabiliano dhidi ya Ebola.

Inaelezwa kwamba ADF linaloundwa na waasi wa zamani wa Uganda, ndilo kundi hatari zaidi kwa raia na limekuwa likitekeleza mashambulizi yake North Kivu na Ituri.

Katika jitihada za kukabiliana na Kundi hilo, DRC na Uganda zimetuma wanajeshi wake kuingia eneo hilo, ingawa bado hakuna mafanikio yaliyopatikana.

Related articles

Recent articles