BUDAPEST, Hungary
MAMLAKA za Hungary zimenasa kitita cha takribani Dola milioni 20 [zaidi ya Sh bil. 52 za Tanzania] zikiwa zimefichwa wakati wa upekuzi uliofanyika dhidi ya Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Viktor Orban.
Upekuzi huo ni sehemu ya operesheni ya kufichua rushwa iliyoanzishwa na Waziri Mkuu wa sasa, Peter Magyar, ambaye alimbwaga Orban katika Uchaguzi wa Aprili, 2026.
Wapekuzi waliweza kubaini sehemu ya fedha zikiwa zimefukiwa kwenye mashimo, majengo na nyumba za kuishi za mwanasiasa huyo.
Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha wa Hungary, Andras Karman, watumishi 12 wa Hazina ya Serikali walitumia muda usiopungua saa nane kuhesabu fedha walizokuta zimefichwa kwa Mstaafu huyo.
Taarifa zinaeleza kuwa sehemu ya fedha hizo zilifichwa kwenye mashimo ili kuhakikisha mamlaka hazizioni.
Kwa upande wake, mamlaka zimesema fedha zilizopatikana zimerejeshwa serikalini na kuwekwa kwenye akaunti ya Hazina.


