MADRID, Hispania
MLINDA mlango wa FC Andorra ya Hispania, Jesus Owono, amefungiwa mechi 12 zikiwa ni siku chache tu tangu aliposababisha kifo cha mshambuliaji wa Tenerife, Jesus de Miguel.
Katika mchezo huo wa Ligi Daraja la Pili nchini Hispania uliochezwa Novemba 2, 2026, Owono mwenye umri wa miaka 25 alilimwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu mbaya De Miguel aliyekimbizwa hospitali na kupoteza maisha siku inayofuata.
Sasa, katika taarifa yake, Kamati ya Nidhamu ya Ligi hiyo imeeleza kuwa imefikia uamuzi wa kumfungia kipa huyo mechi 12 baada ya kupitia ripoti ya mwamuzi wa mechi hiyo.
Katika hatua nyingine, Kamati imeweka wazi kwamba mechi hiyo iliyovunjika zikiwa zimebaki dakika saba baada ya tukio hilo haitorudiwa, hivyo matokeo ya sare ya mabao 2-2 yatabaki vilevile.
Hivi karibuni, kocha wa FC Andorra, Carles Manso, alisema bado Owono raia wa Guinea ya Ikweta hajathibitisha kama atarejea kwenye soka au atastaafu kwa tukio hilo.


