LONDON, Uingereza
KLABU ya Arsenal imetenga dau nono la kumsajili mshambuliaji wa AC Milan, Alphadjo Cisse, kwa mujibu wa mtandao wa Tuttomercatoweb.
Mtandao huo umeitaja Arsenal kuwa mstari wa mbele, licha ya Brighton nayo kuingia kwenye mBio za kumsajili nyota huyo.
Milan wako tayari kumuuza mchezaji huyo lakini kwa sharti la kuwekewa mezani kitita cha Pauni milioni 42 [zaidi ya Sh bil. 14 za Tanzania].
Cisse [20], alianza safari yake ya soka akiwa na Hellas Verona ya Italia, kabla ya kusajiliwa na atanzaro, na hatimaye Milan kumnasa Februari, 2026.
Oktoba, 2026, nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 alifunga ‘hat-trick’ wakati Milan ilipoibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya RB Salzburg katika mchezo wa Ligi ya Europa.


