7.5 C
New York

Alexander-Arnold kurudi Liverpool? Romano akanusha

Published:

MADRID, Hispania

MWANDISHI wa habari za michezo, hasa masuala ya usajili, Fabrizio Romano, amekanusha taarifa zinazodai kuwa beki wa Real Madrid, Trent Alexander-Arnold, ataondoka klabuni hapo Januari, 2027.

Taarifa za awali zilieleza kuwa mlinzi huyo wa kulia raia wa England, atatimka Santiago Bernabeu na kurejea Liverpool wakati huo wa usajili wa dirisha dogo.

Alexander-Arnold alisajiliwa na Madrid akitokea Liverpool mwaka 2025 lakini kwa sasa amepoteza uhakika wa namba chini ya kocha mpya, Jose Mourinho.

Hivi karibuni, mkongwe wa Chelsea, Glen Johnson, aliishauri klabu yake hiyo kuweka mkwanja mezani na kumsajili staa huyo ifikapo Januari.

Hata hivyo, Romano raia wa Italia, ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kusisitiza kuwa Alexander-Arnold hana mpango wa kuondoka Madrid.

Related articles

Recent articles