5 C
New York

Abiria 40 wanusurika kifo ajali basi la Abood

Published:

Na mwandishi Wetu, Gazetini – SHINYANGA

ABIRIA zaidi ya 40 wamenusurika kifo baada ya basi la Abood lenye namba za usajili T285EAV lililokuwa likisarifi kutoka Dar es salaam kwenda Kagera kuwaka moto.

Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo Novemba 13, 2026, katika Kata ya Isaka, Halmashauri ya Msalala, wilayani Kahama, Shinyanga.

Hata hivyo, Mkuu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Wilaya ya Kahama, Stanley Luhwago, amesema walifanikiwa kuuzima moto huo.

“Tumefanikiwa kuuzima moto, hakuna vifo wala majeruhi, abiria wote wametoka salama,” amesema Luhwago.

Kuhusu chanzo cha moto huo na thamani ya mali zilizoharibika, Luhwago amesema uchunguzi bado unaendelea.

Related articles

Recent articles