13.8 C
New York

Ghana yazindukia Somalia, Ayew akosa penalti

Published:

ACCRA, Ghana

TIMU ya soka ya Taifa ya Ghana ‘Black Stars’ imezoa pointi tatu baada ya kupata ushindi wa nyumbani wa mabao 2-0 dhidi ya Somalia katika mchezo wa kufuzu fainali zijazo za Mataifa Afrika [AFCON 2027].

Black Stars wamerudi kwenye reli baada ya kufungwa na Ivory Coast na Gambia katika michezo miwili ya awali ya Kundi C, matokeo yaliyohitimisha kibarua cha kocha Carlos Queiroz.

Katika mechi ya leo Novemba 12, 2026, Ghana wameifunga Somalia wakiwa chini ya kocha wa timu ya wanawake, Kim Bjorkegren, aliyeajiriwa kuchukua nafasi ya Mreno huyo.

Black Stars walipata penalti ya mapema [Dk. 14] lakini staa wake, Jordan Ayew, alishindwa kukwamisha mpira kimiani.

Hata hivyo, bado wenyeji waliweza kupata mabao mawili kupitia kwa Jonas Adjetey na Felix Afena-Gyan.

Related articles

Recent articles