14.8 C
New York

Staa Nigeria azitaka pointi sita za Stars

Published:

LAGOS, Nigeria

NYOTA wa timu ya soka ya Taifa ya Nigeria ‘Super Eagles, Samson Tijani, ameeleza kiu yake ya kuzizoa pointi zote sita za michezo miwili dhidi ya Taifa Stars.

Super Eagles wataivaa Stars leo Novemba 13, 2026, wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao uliopita wa kufuzu fainali za AFCON 2027 dhidi ya Guinea-Bissau.

Katika mahojiano yake kuelekea mechi hiyo, Tijani amesema lengo si tu kushinda mechi ya leo, bali pia kupata pointi zote sita [nyumbani na ugenini] dhidi ya Stars.

Nahodha huyo wa zamani wa timu ya vijana ya U-17 ya Nigeria, anakipiga katika klabu ya Dukla Prague inayoshiriki Ligi Kuu ya Jamhuri ya Czech.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kwa sasa, ameshacheza mechi tatu za timu ya wakubwa ya Nigeria.

“Nataka kujitoa sana kwa ajili ya timu,” amesema na kuongeza: “Muhimu hapa ni kupata pointi zote sita. Nyumbani na ugeni.”

Related articles

Recent articles