LONDON, Uingereza
KLABU ya Crystal Palace imemfuta kazi kocha Pierre Sage, zikiwa ni siku chache tu baada ya timu hiyo kufungwa na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England [EPL].
Palace ‘Eagles’ wametangaza uamuzi huo leo Novemba 12, 2026, kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.
Sage ameondoka na benchi lake la ufundi, wakiwamo waliokuwa makocha wasaidizi watatu; Jamal Alioui, Damien Della Santa na Sandy Guichard.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 47, aliajiriwa na Palace miezi michache iliyopita na kupewa mkataba wa miaka mitatu.
Kilichomponza ni mfululizo wa matokeo mabaya ya timu hiyo msimu huu wa EPL, ambapo imeshinda mechi mbili tu kati ya 10 na inaburuza mkia kwenye msimamo wa Ligi.


