Na mwandishi wetu, Gazetini – DAR
NOVEMBA 6, 2026, Tundu Lissu ambaye ni kiongozi wa CHADEMA, Chama kikuu cha upinzani nchini, alihukumiwa kifungo cha miaka minne gerezani kwa kosa la uchochezi uliotajwa kusababisha machafuko katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Uchochezi? Ndiyo, ni kosa tofauti na lile la uhaini alilokuwa ameshitakiwa nalo, ambalo kama angekutwa na hatia, basi angekumbana na hukumu ya kifo.
Lissu alisema mahakama ilitoa uamuzi huo kwa shinikizo la Serikali, pia akipinga hukumu aliyopewa kwa hoja kwamba haikutokana na mashitaka yaliyokuwa yakimkabili ya uhaini.
SAFARI YA GEREZANI
Kwa miaka mingi, Lissu amejijengea heshima kubwa kwenye siasa za upinzani kwa mtindo wake wa kuikosa bila uoga Serikali na Chama tawala, CCM, hivyo kujikuta mara kadhaa akiingia kwenye mikono ya vyombo vya dola.
Mwaka 2017, alinusurika kifo, japo haimaanishi wahusika ni Serikali, baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha nyumbani kwake mjini Dodoma. Ni shambulizi lililomwachia majeraha kadhaa kwenye mwili wake.
Aprili, 2025, akiwa na ushawishi mkubwa, hasa kuelekea mipango yake ya kugombea urais wa Oktoba, Lissu alikamatwa mjini Mbinga, Iringa, kwa madai ya kuhamasisha wananchi kususia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba. Akafunguliwa kesi ya uhaini.
Kama Ushahidi wa kisheria, waendesha mashitaka walitumia video za mitandaoni zilizomuonesha Lissu akiwataka Watanzania kuupa kisogo Uchaguzi kwa madai ya kuwapo kwa ‘figisu’ kwenye mchakato huo wa kidemokrasia.
Matokeo yake, huku akiendelea kusota gerezani, Uchaguzi ulifanyika Oktoba 29 bila ushiriki wa Chama kikuu cha upinzani, CHADEMA. Uchaguzi uliogubikwa na vurugu, huku vyombo vya dola vikishutumiwa kwa mauaji ya raia.
Francis Ibrahim, mchambuzi wa siasa wa kujitegemea mkazi wa Dar es Salaam, amehojiwa na DW na kusema: “Lawana zinapaswa kwenda kwa vyombo vya dola vilivyokithirisha mamlaka yao na watu waliofadhili, kupanga na kuratibu [vurugu hizo.”
Baada ya vurugu za Uchaguzi, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyekuwa akiwania muhula wake wa pili, alitangazwa mshindi kwa takwimu za asilimia 98 ya kura zilizopigwa na wananchi.
KWANINI SI UHAINI?
Licha ya kushitakiwa kwa uhaini, Lissu alihukumiwa kwa uchochezi. Hii ina maana gani? Mchambuzi wa siasa, Ibrahim, anaamini kilichofanyika ni kuepuka joto kali la kisiasa, ambalo lingeweza kusababishwa na hukumu ya kifo kwa Lissu katika mashitaka ya awali ya uhaini.
Kwa wachambuzi walio wengi, kuhukumiwa kwa uchochezi kunampa nafasi Lissu kukata rufaa, hivyo kuwapo kwa matumaini ya kumuona akirejea uraini, tofauti na ambavyo angehukumiwa kunyongwa kwa uhaini.
Kwa upande wake, viongozi wa CHADEMA wameweka wazi nia yao ya kukata rufaa kupinga kile kilichoamuliwa mahakamani siku hiyo ya Novemba 6.
Hata hivyo, kwa Naibu Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ruqaya Mohammed, kesi ya Lissu ni matokeo ya siasa mbaya. “Siasa zetu ziko zinaelekea gizani,” amesema.
“Nafikiri ni wakati mwafaka sasa, kama Taifa kuwa na mjadala juu ya baadhi ya marekebisho ya sheria na kiuchaguzi. Kama tutaweza, labda tunaweza kuona mwanga.”
NB: GAZETINI imefasiri makala haya kwa lugha ya Kiswahili ikiyatoa kwenye tovuti ya DW yalikokuwa yameandikwa kwa Kiingereza.


