PRETORIA, Afrika Kusini
SIKU chache baada ya kupata ushindi mwembamba katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliomalizika hivi karibuni, viongozi wa Chama tawala nchini Afrika Kusini, African National Congress [ANC], wamekutana kujadili anguko hilo.
Wakati huo huo, Msemaji wa ANC, Mahlengi Bhengu-Motsiri, amesisitiza kuwa Rais Cyril Ramaphosa hatojiuzulu kutokana na aibu hiyo, licha ya vyanzo vingi vya Habari kudai hivyo.
Kikao hicho ni mwitikio wa ushauri wa wadau wa siasa nchini humo waliokitaka Chama hicho kilichopigania uhuru wa Afrika Kusini kujitafakari.
“Kumekuwa na upotoshaji mkubwa kuhusu Rais, kwamba ameamua kujizulu, tunawataka Waafrika Kusini kupuuza …” amesema Bhengu-Motsiri.
Matokeo ya safari hii ni mwendelezo wa kile kilichotokea miaka miwili iliyopita, ambapo ANC ilipoteza wingi wa wawakilishi wake kwenye Bunge la Afrika Kusini.


