15.7 C
New York

Baada ya kichapo, Alonso atupa lawama kwa beki

Published:

LONDON, Uingereza

KOCHA wa Chelsea, Xabi Alonso, amemetupia lawama beki wake, Levi Colwill, baada ya kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Sunderland katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa leo Novemba 8, 2026.

Colwill amebeba lawama kwa rafu aliyomchezea Brian Brobbey iliyosababisha Sunderland kupewa mkwaju wa penalti na kufunga bao pekee hilo.

Tukio hilo la kumwangusha Brobbey lilimlazimisha mwamuzi wa kati kutumia VAR iliyotoa majibu kwamba ulipaswa kuwa mkwaju wa penalti.

Wakati huo huo, Alonso amesema kwa ujumla vijana wake walishindwa kuendana na kasi ya mchezo. “Ni kosa letu … Tulikosa kasi tukiwa na mpira, hatukutengeneza nafasi za kufunga,” amesema.

Kwa mchezo huo, ni wazi sasa kocha Alonso ana kazi kubwa mbili; kuimarisha safu ya ushamhuliaji, pamoja na kufanyia kazi mapungufu ya ‘ukuta’ wake.

Related articles

Recent articles