14.2 C
New York

Wahalifu wa mitandao wamdukua Waziri, Urusi yatajwa

Published:

MILAN, Italia

WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Italia, Antonio Tajani, amesema wahalifu wa mitandao wamedukua taarifa zake na kuzichapisha kwa sababu tu anaiunga mkono Ukraine katika vita dhidi ya Urusi.

“Kwa siku kadhaa sasa, wahalifu wa mitandao wamekuwa wakiingia na kuona taarifa zangu na kunipa jumbe za vitisho,” ameandika Tajani katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X [zamani Twitter].

Hata hivyo, Waziri huyo hakufunguka zaidi juu ya aina ya vitisho alivyopewa, ingawa amesema familia yake pia imekuwa ikitumiwa jumbe za aina hiyo.

“Kutetea uhuru wa nchi yenye mamlaka kamili, kuwa na msimamo wa kuunga mkono uhuru na demokrasia ya nchi si jambo linalowapendeza wahalifu,” amesisitiza.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni, amewatupia lawama wahalifu hao wanaoiunga mkono Urusi na kusisitiza kuwa yuko bega kwa bega na Tajani.

Hata hivyo, licha ya kuhusishwa na wadukuazi hao, Serikali ya Urusi chini ya Rais Vladmir Putin haijatoa taarifa yoyote ya kupinga au kukiri kuhusika na tukio hilo.

Related articles

Recent articles