RIYADH, Saudi Arabia
CHOMBO cha habari kinachofanya kazi na Kundi la Houthi kimeripoti shambulizi la anga lililofanywa na Saudi Arabia na kuua watu takribani 25 nchini Yemen.
Houthi, kundi la kigaidi la Yemen, limekuwa na uhusiano mbaya na Saudi kwa madai kwamba imekuwa ikiiunga mkono Serikali iliyoko madarakani nchini humo.
Katika video iliyopostiwa na chombo hicho cha habari, Al Masirah, waokoaji wanonekana wakitoa miili ya watu katika majengo mbalimbali mjini al-Shariyah, Mashariki mwa Mji Mkuu wa Sanaa.
Aidha, video zingine zilizosambazwa na Al Masirah zinaonesha majeruhi wakiwa wamebebwa kukimbizwa hospitali.
Serikali ya Saudia, pamoja na ile ya Yemen, zimekuwa na ushirikiano wa miaka zaidi ya 10 kupigana na Houthi.
Kwa miezi ya hivi karibuni, Houthi wanaopewa nguvu na Iran, wameweza kushambulia Uwanja wa Ndege wa Abha nchini Saudia, kisha kulenga meli zake za mafuta.


