13.4 C
New York

Staa Al Ahly aingia rada za Atletico

Published:

MADRID, Hispania

MWANDISHI wa habari za michezo nchini Misri, Moham Mamdouh, amesema Atletico Madrid inamtolea macho winga wa Al Ahly ya Misri, Youssef Abdullah.

Katika mahojiano yake na ON Sport, Mamdouh ameeleza kuwa Atletico wamekuwa wakimfuatilia Abdullah baada ya kuvutiwa na kiwango alichokionesha wakati wa fainali za Kombe la Dunia za U-17.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali kutoka Misri, Al Ahly haijapokea ofa yoyote kutoka Atletico lakini huenda klabu hiyo ya Hispania ikafika mezani Februari, 2027.

Abdullah alitokea katika ‘academy’ ya Pyramid, kabla ya kujiunga na Al Ahly na hivi karibuni alikuwa sehemu ya kikosi cha U-17 ya Misri kilichotwaa ubingwa wa Gulf Cup nchini Qatar.

Nyota huyo atakuwa kinda wa pili wa Al Ahly kutua Hispania kwa siku za hivi karibuni baada ya Hamza Abdelkarim kusajiliwa na Barcelona mapema mwaka huu.

Related articles

Recent articles