13.4 C
New York

Allegri awekwa kitimoto Napoli

Published:

NAPOLI, Italia

MMILIKI wa klabu ya Napoli, Aurelio De Laurentiis, hivi karibuni alifika kwenye uwanja wa mazoezi na kikao cha dharura na kocha Massimiliano Allegri, wasaidizi wake wa benchi la ufundi na wachezaji.

Kikao cha bosi hicho kinakuja baada ya Allegri kupoteza mechi saba kati ya 14 alizokaa kwenye benchi msimu huu wa 2026-27.

Napoli imetoka kupoteza mechi mbili mfululizo, ikitandikwa mabao 4-1 na Juventus, kisha kuchezea kichapo kama hicho mbele ya wakali wa Ureno, Porto.

Kwa sasa, timu hiyo inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa Serie A baada ya kucheza mechi 10, ikiwa imeachwa pointi 14 na vinara wa Ligi.

Wakati huo huo, Napoli inakamata nafasi ya 27 kwenye msimamo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa na pointi tatu tu baada ya mechi zake nne.

Related articles

Recent articles