LONDON, Uingereza
REAL Madrid na PSG zimeingia kwenye vita ya kuiwania saini ya mlinda mlango wa Aston Villa, Zion Suzuki, baada ya kiwango chake kizuri chini ya kocha Unai Emery.
Suzuki [24], alisajiliwa na Villa katika dirisha la usajili wa kiangazi lililopita ili kuchukua nafasi ya Emi Martinez aliyeondoka na kutimkia Chelsea.
PSG walijaribu kumsajili kipa huyo raia wa Japan lakini walibadili maamuzi na hatimaye akajiunga na Villa.
Madrid, licha ya kutaka kumpa mkataba mpya Thibaut Courtois, bado wanahitaji kipa wa kumsaidia majukumu.
Kwa upande mwingine, klabu za Arsenal, Liverpool na Manchester City nazo zimeripotiwa kuitaka saini ya mlinda mlango huyo.


