21 C
New York

Infographic| Kilimo; Utajiri unaokumbwa na vikwazo lukuki

Published:

Kwa mujibu wa Matokeo ya Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Mwaka wa Kilimo 2019/2020 yanaonyesha kuwa, kaya nyingi zilikutana na vikwazo mbalimbali katika Mwaka wa Kilimo 2019/20.

Kati ya vikwazo vingi vilivyoripotiwa, baadhi ya vikwazo vikubwa muhimu vilivyoripotiwa na kaya katika shughuli za kilimo ni mabadiliko ya tabianchi (ukame, mafuriko; asilimia 17.8).

Gharama za pembejeo (asilimia 15.6), upatikanaji wa ardhi (asilimia 13.5), bei ndogo za mazao (asilimia 7.2), magonjwa na wadudu waharibifu (asilimia 6.7), upatikanaji wa pembejeo (asilimia 5.6) na rutuba ya udongo (asilimia 5.6).

Hali kwa Tanzania Bara

Hata hivyo, Pamoja na changamoto hizo, vikwazo katika Kilimo, kwa upande wa Tanzania Bara matokeo yanaonesha kuwa, mabadiliko ya tabianchi (ukame, mafuriko; asilimia 18.1) yaliathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za sekta ya kilimo, ikifuatiwa na gharama za pembejeo (asilimia 15.8).

Pia kulikuwa na bei ndogo za mazao (asilimia 7.4), upatikanaji wa ardhi (asilimia 13.6), bei ndogo za mazao (asilimia 7.4), magonjwa na wadudu waharibifu (asilimia 6.6), upatikanaji wa pembejeo (asilimia 5.6) na rutuba ya udongo (asilimia 5.4).

Hali kwa Tanzania Zanzibar

Kwa upande wa Tanzania Zanzibar, matokeo ya Sensa yanaonesha kuwa, wizi wa mazao (asilimia 20.8) ni kikwazo kikubwa kilichoathiri shughuli za kilimo kwa mwaka wa kilimo 2019/20, ikifuatiwa na upatikanaji wa ardhi (asilimia 12.0).

Aidha, uharibifu wa wanyama/ndege (asilimia 11.0), magonjwa na wadudu waharibifu (asilimia 11.0), gharama za pembejeo (asilimia 6.8), upatikanaji wa pembejeo (asilimia 5.1) na wizi wa mifugo (asilimia 5.1).

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img