8.9 C
New York

Hakimi awaweka njiapanda PSG

Published:

PARIS, Ufaransa

BEKI wa kulia wa PSG, Achraf Hakimi, anawapa wakati mgumu mabosi wa klabu hiyo baada ya kuwaambia wasubiri kuhusu mazungumzo ya mkataba mpya.

Uongozi wa PSG ulishaanza kuwasiliana na wakala wake kujadili mkataba mpya lakini mlinzi huyo raia wa Morocco akawaambia hakuna haja ya kuharakisha.

Mkataba wake wa sasa na klabu hiyo ya Paris utafikia ukomo Juni, 2029, lakini mabosi walitaka kumpa mwingine wa muda mrefu.

Kitendo cha Hakimi kuwasubirisha kinawaumiza vichwa viongozi wa PSG wakiamini huenda mlinzi huyo ameshaanza kufikiria mpango wa kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Klabu za Ligi Kuu ya Saudi Arabia, pamoja na zile za Uturuki, zimekuwa zikihusishwa na saini ya beki huyo, huku taarifa kutoka Ufaransa zikidai kuwa anataka kubaki Ulaya.

Related articles

Recent articles