16.6 C
New York

Rihanna amshukia Donald Trump

Published:

LOS ANGELES, Marekani

STAA wa muziki wa Pop na R&B, Rihanna, amewajia juu wananchi wa Marekani ambao hawakupiga kura wakati Rais Donald Trump anashinda kiti cha urais mwaka 2024.

Rihanna amedai kuwa wao ndiyo wanaopaswa kulaumiwa kwani walisababisha Trump kuibuka mshindi na kuingia kwa awamu ya pili madarakani.

Trump alishinda kiti cha urais kwa kumbwaga mgombea wa urais wa Democratic, Kamala Harris. Alirejea Ikulu baada ya kuangushwa na Joe Biden katika Uchaguzi wa mwaka 2020.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Rihanna amedai kuwa ambao hawakupiga kura ndiyo wa kulaumiwa kwa hiki kinachoendelea.

Utawala wa Trump unakabiliwa na ukosolewaji mkubwa, hasa kwa ugumu wa maisha unaolalamikiwa na wananchi walio wengi.

“Amini, usiamini. Wale ambao hawakupiga kura ndiyo waliosababisha haya,” amesema Rihanna kupitia Instagram.

Related articles

Recent articles