16.6 C
New York

Ajali ya treni yaua 68, Waziri afunguka chanzo

Published:

MADRID, Hispania

WATU takribani 68 wamepoteza maisha baada ya treni mbili za umeme kugongana huko Kusini mwa Jiji la Madrid.

Taarifa zinaeleza kuwa hiyo ni ajali mbaya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo tangu mwaka 2013.

Waziri wa Usafirishaji wa Hispania ameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kupoteana kwa mawasiliano kati ya treni hizo.

Akifafanua zaidi, amesema tatizo lilianzia pale kompyuta za kituo cha kuziongoza treni hizo iliposhindwa kufanya kazi.

Kwa upande wake, muongozaji wa reli, Iryo, amesema abiria zaidi ya 500 walikuwa kwenye treni mbili hizo.

Related articles

Recent articles