LONDON, Uingereza
KLABU ya PSG imeingia kwa nguvu zote katika mBio za kuiwania saini ya kiungo wa pembeni wa Chelsea, Estevao.
PSG wamemgeukia nyota huyo wakiamini anawafaa kuziba pengo la Khvicha Kvaratskhelia aliyepata majeraha.
Hivi karibuni, PSG walihusishwa kumfuatilia winga wa Bayer Leverkusen, Ibrahim Maza, ambaye pia ni kiungo mshambuliaji.
Estevao alisajiliwa na Chelsea kwa Pauni milioni 38 mwaka 2025 lakini kwa sasa haonekani dili mbele ya kocha Xabi Alonso.
Licha ya kuonesha kiwango kizuri mara kadhaa, Mbrazil huyo ametumika katika dakika 172 pekee katika mechi nane alizocheza.


