PARIS, Ufaransa
MKUU wa Maendeleo ya Soka wa Shirikisho la mchezo huo duniani [FIFA], Arsene Wenger, ameitaka Afrika kutwaa Kombe la Dunia.
Wenger, kocha wa zamani wa Arsenal, ameibuka na ushauri huo wakati wa Mkutano Mkuu wa Kimkakati wa Shirikisho la Soka barani Afrika [CAF] uliofanyika Santa Maria, Cape Verde.
Kwa mujibu wa Mfaransa huyo, takwimu zilizopo zinaonesha kuwa Afrika inaweza kuwa bingwa wa fainali hizo.
Alikumbushia pia timu tisa kati ya 10 zilizoshiriki Kombe la Dunia mwaka huu [2026] zilivuka hatua ya makundi.
“Katika fainali hizo, ilikuwa ngumu sana kuzifunga timu za Afrika kutokana na nidhamu na kiwango chao kimefikia kiwango cha juu,” amesema.


