15.5 C
New York

Magonjwa ya upumuaji yashika kasi Indonesia

Published:

JAKARTA, Indonesia

WATU takribani 175,000 nchini Indonesia wameripotiwa kukabiliwa na magonjwa ya upumuaji, ikiwamo pneumonia.

Idadi hiyo, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Indonesia, ni ndani ya mwezi mmoja, yaani kuanzia Agosti, 2026, hadi sasa.

Ikifafanua zaidi, taarifa ya Wizara imeeleza kuwa changamoto hiyo ya magonjwa ya upumuaji imetokana na majanga ya moto ya misituni. Kati ya hao 175,000, Wizara imedai kuwa zaidi ya 40,000 ni watoto.

Indonesia imetumia wataalamu 54,000 na ndege kadhaa zisizo na rubani kukabiliana na moto wa misituni katika Visiwa vya Borneo na Sumatra.

Aidha, Majanga ya moto misituni si tu yameikumba Indonesia, bali pia yamejitokeza katika nchi Jirani za Malaysia na Singapore.

Related articles

Recent articles