18.3 C
New York

Rodri apanga usajili Barcelona

Published:

CATALUNYA, Hispania

KIUNGO wa Barcelona, Rodri, ametaja maeneo yanayopaswa kufanyiwa kazi ili kuboresha kikosi hicho wakati wa usajili wa kiangazi, 2027.

Rodri ameibuka na ushauri huo baada ya Barcelona kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Galatasaray katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya

“Kwa mfano, [Galatasaray] walipopata bao la kwanza, wangeweza pia kufunga jingine. Lazima tuimarishe eneo hilo [ulinzi],” amesema.

Pia, Mhispania huyo amelitaka benchi la ufundi chini ya kocha Hansi Flick kubadili aina ya uchezaji kwa kuachana na kutegemea mashambulizi ya kushitukiza.

Katika mechi hiyo, Barcelona ilipata mabao yake kupitia kwa Joao Cancelo, Fermín Lopez, Anthony Gordon na Karim Adeyemi.

Wacatalunya hao watarejea dimbani wikiendi hii kwa mchezo wa Ligi Kuu [La Liga] dhidi ya Betis.

Related articles

Recent articles