18.3 C
New York

Mkongwe amchongea Lisandro Martinez

Published:

MANCHESTER, Uingereza

STRAIKA wa zamani wa Ligi Kuu ya England [EPL], Jimmy Floyd Hasselbaink, ameitaka Manchester United kumsimamisha beki wake wa kati, Lisandro Martinez.

Hasselbaink ni miongoni mwa ambao hawajafurahishwa na kitendo cha mchezaji huyo kuukosoa hadharani uongozi wa Man United.

Akihojiwa baada ya Man United kufungwa mabao 2-0 na Atletico Madrid hivi karibuni, Martinez alielekeza lawama kwa mabosi wat imu hiyo akisema hawajafanya usajili mzuri.

Hasselbaink, kwa upande wake, amesema Martinez anapaswa kuadhibiwa kwa kosa la kukosoa viongozi hadharani, badala ya kutumia njia za mawasiliano ya ndani ya klabu.

“Ana hoja lakini unafikiri alikuwa sahihi kusema hayo? Natarajia asitumike katika mechi chache zijazo. Huwezi kuibuka hadharani na kusema aliyosema,” amesema Hasselbaink.

Related articles

Recent articles