MANCHESTER, Uingereza
KLABU ya Manchester City imeripotiwa kuanza mapema mikakati ya kuinasa saini ya mshambuliaji wa Atletico Madrid, Alex Baena.
Kwa mujibu wa ripoti, usajili wa mchezaji huyo utafanyika wakati wa dirisha dogo la Januari, 2027.
Man City ilitumia usajili wa kiangazi uliofungwa hivi karibuni kwa kuimarisha safu yake ya ushambuliaji, ikiwaingiza Allan kutoka Palmeiras na Iliman Ndiaye aliyekuwa Everton.
Wakati huo huo, iliwanasa Mathys Detourbet na Jeremy Monga, ambao hata hivyo wametolewa kwa mkopo katika klabu za Monaco na Swansea City.
Sasa, mtandao wa Caught Offside umeripoti kuwa Man City ni moja ya klabu tatu za Ligi Kuu ya England zinazomtaka Baena.


