LONDON, Uingereza
CHELSEA ilikuwa na nafasi ya kumsajili Yves Bissouma baada ya kiungo wake, Enzo Fernandez, kutimkia kwa washindano wao wa Ligi Kuu ya England, Manchester City.
Bissouma ni mchezaji huru baada ya kuondoka Tottenham iliyomsajili mwaka 2022 akitokea Brighton.
Mtandao wa SunSport umeeleza kuwa nyota huyo raia wa Mali alipokea ofa za Ajax na Monaco lakini alizikataa akisisitiza kuwa anataka kubaki England.
Chelsea walikuwa na nafasi ya kumsajili na zipo taarifa kuwa yalishafanyika mazungumzo ya pande mbili juu ya uhamisho wake.
Hata hivyo, Blues walizembe dakika za mwisho wakidhani wamefanikiwa kuinasa saini ya kiungo wa Monaco, Lamine Camara.


