21.3 C
New York

Pellegrini aibuka kumjibu Mourinho

Published:

MADRID, Hispania

KOCHA wa Real Betis, Manuel Pellegrini, hajafurahishwa na kauli ya Jose Mourinho baada ya mchezo wa La Liga wa jana Septemba 4, 2026.

Baada ya dakika 90 za mechi hiyo iliyomalizika kwa Betis kushinda bao 1-0, Mourinho alidai kuwa ni bahati tu iliyowabeba wapinzani wao kupata pointi tatu.

Katika mahojiano yake na waandishi wa habari, Mourinho alisema Betis ilicheza kwa kujihami ili walau kupata sare tu.

Akimjibu, Pellegrini alisema: “Sitosema alichokiona lakini nafikiri tulistahili ushindi tangu dakika ya kwanza ya mchezo.”

Wakati huo huo, kocha huyo wa kimataifa wa Chile alimpongeza kipa wake, Alvaro Valles, akisema alifanya kazi nzuri, hasa kuokoa mipira mitatu ya hatari iliyotokana na faulo.

Related articles

Recent articles